• HABARI MPYA

  Wednesday, March 27, 2019

  KMC NA LIPULI FC ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za KMC ya Kinondoni na Lipuli ya Iringa leo zimefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi dhidi ya wapinzani wao.
  KMC imeichapa 2-0 African Lyon katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Dar es Salaam mabao ya Mohamed Rashid dakika ya 47 na Cliff Buyoya dakika ya 88.
  Nayo Lipuli FC imeichapa Singida United 2-0 pia, mabao ya Jimmy Shoji dakika ya 33 na Haruna Shamte dakika ya 90.

  Kwa matokeo hayo, KMC itamenyana na mshindi kati ya Kagera Sugar na Azam FC zitakazomenyana keshikutwa, Ijumaa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Lipuli FC itamenyana na mshindi kati ya Alliance FC na Yanga SC zitakazomenyana Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC NA LIPULI FC ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top