• HABARI MPYA

  Wednesday, March 27, 2019

  LUKUMAY NA NYIKA ‘WABWAGA MANYANGA’ YANGA WAMKABIDHI TIMU KAPTENI MKUCHIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIONGOZI wawili waliokuwa wamebaki madarakani Yanga SC, kaimu Mwenyekiti Samuel Lukumay na Mjumbe, Hussein Nyika wametangaza kujiuzulu nafasi zao leo mjini Dar es Salaam ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
  Akizungumza makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam leo, Lukumay alisema kwamba baada ya uamuzi huo, wanaikabidhi timu kwa Baraza la Wadhamini chini ya Mwenyekiti, Kapteni George Huruma Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  Lukumay amesema wamelazimika kujiuzulu baada ya Wajumbe wenzao wawili, Siza Lyimo na Thobias Lingalangala kujiuzulu wiki mbili zilizopita na kufanya klabu ibaki na viongozi wawili tu  kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam, ambao ni yeye na Nyika.

  Samuel Lukumay ametangaza kujiuzulu Yanga SC mjini Dar es Salaam leo ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu

  “Kikubwa kilichotusababihsa tufanye hivi, ni kwamba nadhani wiki moja mbili zilizopita, tulikuwa tumebaki wajumbe wanne, lakini wenzetu wawili walijiuzulu hiyvo uchaguzi mdogo ungekuwa wa kujaza nafasi sita,”amesema Lukumay. 
  Amesema sasa Baraza la Wadhamini na Sekretarieti ya klabu watashirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuendesha mchakato wa Uchaguzi Mkuu ambao unaanza upya.  
  Wengine waliojiuzulu ni Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe Inspekta Hashim Abdallah, Salum Mkemi, Omary Said na Ayoub Nyenzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKUMAY NA NYIKA ‘WABWAGA MANYANGA’ YANGA WAMKABIDHI TIMU KAPTENI MKUCHIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top