• HABARI MPYA

  Tuesday, March 19, 2019

  WANNE SIMBA WAITWA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE, YANGA ACHUKULIWA MMOJA TU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NYOTA wanne wa Simba Queens wameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 27 timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kujiandaa na mchezo wa kufuzu Olimpiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwakani mjini Beijing, China.
  Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo imewataja wachezaji hao ni Mwanahamis Omari Shurua ‘Gaucho’, Amina  Ally Bilal, Dotto Evarist Tossy na Amina Abdallah.
  JKT Queens imeendelea kuwa timu yenye mchango mkubwa Twiga Stars baada ya kutoa wachezaji 12 ambao ni Fatuma Omar Jawadu, Najiath Abbas Idrissa, Maimuna Hamisi Kaimu, Fatuma Khatibu Salumu, Happyness Hezron Mwaipaja, Stumai Abdallah Athumani, Anastazia Antony Katunzi, Fatuma Bushir Makusanya, Zena Khamis Rashid, Donisia Daniel Minja, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Fatuma Mustapha Swalehe.

  Alliance Queens ya Mwanza imetoa wachezaji watatu ambao ni Enekia Yona Kasonga, Aisha Khamis Masaka na Esther Mabanza Gindlya sawa na Kigoma Sisters iliyowatoa Gelwa Lugomba Yona, Asha Shaaban Hamza na Irene Elias Kisisa, wakati Mlandizi Queens imetoa wachezaji wawili ambao ni Wema Richard Maile na Tausi Abdallah Salehe.
  Yanga Princess yenyewe imetoa mchezaji mmoja tu kwenye kikosi cha Twiga Stars ambaye ni Grace Tony Mbelay sawa na Evergreen iliyomtoa Fatuma Issa Maonyo ‘Densa’ na Marsh Academy ya Mwanza iliyomtoa Niwael Khalfan Makuruta.
  Kikosi cha Twiga Stars kinachonolewa na kocha Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ anayesaidiwa na Edna Lema kinatarajiwa kuingia kambini Jumatano kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu Olimpiki upande wa soka ya wanawake.
  Na mchezo wa kwanza umepangwa kuchezwa Aprili 5 mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 9 mjini Kinshasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WANNE SIMBA WAITWA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE, YANGA ACHUKULIWA MMOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top