• HABARI MPYA

  Friday, March 29, 2019

  MSUVA AIFUNGIA BAO LA KUSAWAZISHA DIFAA EL-JADIDI YATOA SARE 1-1 NA WYDAD CASABLANCA

  Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA 
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana aliinusuru timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi kupoteza mchezo wa ugenini wa wa Ligi Kuu ya Morocco kwa kuisaidia kutoa sare ya 1-1 na Wydad Casablanca katika.
  Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC, aliifungia Difaa Hassan El-Jadidi bao la kusawazisha dakika ya 68 ikitoa sare ya 1-1 na Wydad Casablanca katika mchezo huo wa Ligi Morocco, maarufu kama Botola Pro uliokuwa mkali na wa kusisimua.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi huko El Jadida mjini Mazghan, Wydad walitangulia kwa bao la kiungo Mnigeria, Michael Babatunde dakika ya kabla ya Msuva mwenye umri wa miaka 25 kuisawazishia Difaa Hassan El-Jadidi dakika ya 68.
  Simon Msuva akishangilia baada ya aliinusuru Difaa Hassan El-Jadidi kupoteza mchezo dhidi ya Wydad Casablanca jana

  Simon Msuva akiwa chini ya ulinzi wa beki wa Wydad Casablanca jana 

  Simon Msuva wa kwanza kulia mbele katika kikosi cha Difaa Hassan El-Jadidi kilichotoa sare na Wydad Casablanca jana

  Kwa matokeo hayo, Difaa Hassan El-Jadidi inajiongezea pointi moja na kufikisha 26 baada ya kucheza mechi 22, ingawa inabaki nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16, ikiizidi pointi saba tu Kawkab Marrakech inayoshika mkia Botola Pro.
  Wydad Casablanca, mabingwa wa zamani wa Afrika na wana Robo Fainali msimu huu, wenyewe baada ya sare ya jana wamefikisha pointi 49 katika mchezo wa 22 na kuendelea kuongoza Botola Pro kwa pointi 16 zaidi ya Hassania Agadir na Ittihad Tanger wanaofuatia wakiwa wamefungana kwa pointi 33 kila timu.
  Msuva alikuwa anacheza mechi ya kwanza tu Difaa Hassan El-Jadidi tangu arejee kutoka nchini kwake, Tanzania ambako Jumapili aliiwezesha timu yake ya taifa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Juni mwaka huu nchini Misri kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi L mjini Dar es Salaam.
  Siku hiyo Msuva alifunga bao la kwanza kabla ya mkongwe,Erasto Edward Nyoni kufunga la pili na beki mwingine, Aggrey Morris kufunga la tatu Uwanja wa Taifa na Tanzania ikifuzu AFCON ya pili tu kihistoria baada ya ile ya mwaka 1980 Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AIFUNGIA BAO LA KUSAWAZISHA DIFAA EL-JADIDI YATOA SARE 1-1 NA WYDAD CASABLANCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top