• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 28, 2019

  SOLSKJAER ASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU MAN UNITED

  Ole Gunnar Solskjaer amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea na kazi Manchester United   MANCHESTER UNITED CHINI YA SOLSKJAER 

  Mechi ilizocheza: 19
  Mechi iliozshinda: 14
  Mechi ilizotoa sare: 2
  Mechi ilizofungwa: 3
  Mechi za bila kuruhusu bao: 7
  Asilimia ya ushindi: 74
  Mabao iliyofunga: 40
  Bao kwa mchezo: 2.11
  Mabao iliyoruhusu: 17
  Mabao ya kuruhus kwa mchezo: 0.89
  KOCHA Ole Gunnar Solskjaer amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea na kazi Manchester United baada ya kufanya kazi kama kocha wa muda. 
  Gwiji huyo wa Norwegian, ambaye alirejea Old Trafford mwezi Desemba, amepewa baraka na Ed Woodward na familia ya Glazer baada ya kuiongoza timu kushinda mechi 14 kati ya 19. 
  Inafahamika kwamba Solskjaer alipewa mkataba wa kuwa kocha wa muda mrefu wa mapema wiki hii katika mkutano wa ana kwa ana na Mwenyekiti Woodward Uwanja wa mazoezi wa klabu. 
  Mkataba wake una thamani ya Pauni Milioni 7 kwa mwaka, pungufu ya zaidi ya nusu kutoka Pauni Milioni 18 ambazo inaaminika klabu inamlipa mtangulizi wa Mnorway huyo, Jose Mourinho.
  Tayari Solskjaer ameanza mikakati ya usajili kuimarisha kikosi mwishoni mwa simu na ameahidiwa fungu la kukamilisha mpango huo. 
  Solskjaer anaweza kuongeza watu kwenye benchi lake la Ufundi, lakini hawezi kuwaondoa Michael Carrick, Kieran McKenna na Emilio Alvarez, ila mustakabali wa Mike Phelan haujulikani.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SOLSKJAER ASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top