• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 14, 2019

  ARSENAL KUFA AU KUPONA LEO ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE


  TIMU ya Arsenal wana kazi kubwa mikononi mwao kama wanataka kuendelea kuuota ubingwa wa Europa mwaka huu.
  Arsenal walipoteza mchezo kwa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya kawaida kabisa kutoka ligi ya Ufaransa kwenye mechi ya kwanza ya mzunguko wa 16 bora wiki iliyopita na kwa sasa sasa wanahitaji walau magoli mawili bila majibu ili kufuzu kwenda hatua ya Robo fainali.
  Vijana wa Unai Emery walipata ushindi muhimu dhidi ya Manchester United jumapili na morali yao imeongezeka maradufu, hata hivyo Arsenal watakuwa bila beki wao Sokratis ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita.
  Kocha huyo anatarajia kumuanzisha mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati dhidi ya Manchester United kwani anahitaji magoli zaidi ya kitu chochote ili aweze kufuzu.
  Kwingineko Chelsea wako katika hali nzuri ukilinganisha na jirani zao wa jiji la London.
  Wao walifunga mabao 3-0 dhidi ya Dynamo Kyiv kwenye mchezo wa kwanza lakini walidondosha alama mbili siku ya jumapili walipokutana na Wolves kwenye ligi – matokeo ambayo yaliwafanya wasirejee katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.
  Kocha Maurizio Sarri anasema, “Ni kombe (Europa) la muhimu sana kwetu. Na kuna nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa kwa bingwa kwa hiyo lengo letu na ni muhimu kwetu kushinda.”
  Napoli ni timu nyingine iliyofanya vizuri wiki iliyopita baada ya kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Red Bull Salzburg, huku timu nyingine kutoka Serie A, Inter Milan ilitoka sare na Frankfurt walipokutana wiki iliyopita.
  Ni StarTimes pekee ndio watakaokuonyesha ligi ya Europa kupitia chaneli zao za michezo. Arsenal vs Rennais saa 5:00 Usiku na utaonyeshwa LIVE kupitia ST World Football, Dynamo Kyiv vs Chelsea saa 2:55 Usiku nao pia utakuwa LIVE kupitia ST World Football.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL KUFA AU KUPONA LEO ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top