• HABARI MPYA

  Monday, March 18, 2019

  HASSAN KESSY ATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, OMDURMAN
  BEKI Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy amefuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na timu yake, Nkana FC kufungwa mabao 4-1 na Al-Hilal Omdurman usiku wa jana Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman katika mchezo wa mwisho wa Kundi C.
  Mabao ya Al-Hilal yalifungwa na Sharaf Eldin Ali dakika ya tano, Waleed Bakhet Hamid mawiloi dakika ya 19 na 61 na Idris Mbombo dakika ya 77, wakati la Nkana lilifungwa na Walter Bwalya dakika ya 48.
  Lakini Hassan Kessy, mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga za Dar es Salaam hakuwepo hata benchi kwenye mchezo wa jana nchini Sudan.

  Hassan Kessy (kushoto) amefuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 

  Al-Hilal inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake 11, ikifuatiwa na Nkana FC yenye pointi tisa, timu nyingine ya Zambia, ZESCO United imeshika mkia kwa pointi zake pamoja na kuifunga Asante Kotoko 2-1 jana.
  Mbali na Al Hilal na Nkana kufuzu Robo Fainali, timu nyingine zilizofuzu ni RSB Berkane na Hassania Agadir zote za Morocco kutoka Kundi A, CS Sfaxien na Etoile du Sahel zote za Tunisia kutoka Kundi B na Gor Mahia ya Kenya na Zamalek ya Misri kutoka Kundi D.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HASSAN KESSY ATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top