MSHAMBULIAJI Walaal Musa jana alikuwa shujaa wa Sudan baada ya bao lake pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Mauritania kuipeleka timu yake Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
Ushindi huo unawafanya Desert Hawks wafuzu Nane Bora wakiungana na wenyeji, Morocco ambao katika mchezo uliotangulia jana waliichapa Guinea 3-1 at Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca.
Sasa Morocco na Sudan kila timu ina pointi sita katika Kundi A, mbele ya Guinea na Mauritania ambazo hazina pointi.
CHAN inaendelea leo kwa mechi za Kundi B, Ivory Coast ikimenyana na Zambia na Uganda watacheza na Namibia.

0 comments:
Post a Comment