• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 30, 2018

  MAN UNITED KUIVAA HUDDERSFIELD AU BIRMINGHAM KOMBE LA FA

  Alexis Sanchez (kulia) alianza kuichezea Manchester United katika Kombe la FA Ijumaa PICHA ZAIDI HAPA
    

  RAUNDI YA TANO YA KOMBE LA FA 

  Sheffield Wednesday v Notts County au Swansea
  West Brom v Southampton
  Chelsea v Hull
  Leicester v Sheffield United
  Huddersfield au Birmingham v Manchester United
  Millwall au Rochdale v Newport or Tottenham
  Brighton v Coventry
  Wigan v Manchester City 
  TIMU ya Manchester United itamenyana na Huddersfield au Birmingham katika Raundi ya Tano ya Kombe la FA England. 
  Hiyo ni baada ya droo iliyopangwa jana na Chama cha Soka England (FA) na Mashetani hao Wekundu watasubiri kujua mpinzani wao baada ya mechi ya marudio baina ya timu hizo.
  Mahasimu wao, Manchester City watasafiri kuwafuata Wigan Athletic Uwanja wa DW katika mchezo mwingine wa Raundi ya Tano Kombe la FA England.
  Vinara hao wa Ligi Daraja la Kwanza, wakitoka kuwatoa West Ham United na AFC Bournemouth katika hatua za mwanzo za mashindano msimu huu, watakutana na timu ya kocha Pep Guardiola yenye rekodi ya kuogopesha.
  Huo unatarajiwa kuwa mchezo wa marudio ya fainali ya Kombe la FA England mwaka 2013 wakati Wigan ilipoifunga Man City 1-0 Uwanja wa Wembley.  
  Wigan ilitwaa Kombe la FA  wakati David Sharpe anatimiza umri wa miaka 22 na akateuliwa kuwa Mwenyekiti wa timu miaka miwili baadaye wakati babu yake, Dave Whelan alipojiuzulu baada ya miaka 20 madarakani.
  Tottenham Hotspur wanaweza kusafiri kuwafuata Millwall ikiwa timu zote zitashinda mechi zake za marudiano za Raundi ya Nne ya Kombe la FA England.
  Mechi za raundi ya tano ya Kombe la FA England zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Februari 17 na 18, mwaka huu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED KUIVAA HUDDERSFIELD AU BIRMINGHAM KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top