• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 24, 2018

  ENGLAND YAPANGWA NA HISPANIA, CROATIA MICHUANO MIPYA UEFA

  TIMU ya taifa ya England imepangwa kundi moja na Hispania na Croatia katika michuano mipya midogo ya Ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA), inayotarajiwa kuanza Septemba mwaka huu.
  Three Lions ya kocha Gareth Southgate ipo kwenye michuano hiyo iliyoanzishwa maalum kupunguza mechi za kirafiki zisizo na maana. 
  Katika Kundi B4, Wales na Jamhuri ya Ireland zimepangwa pamoja —  maana yake kocha Ryan Giggs atakutana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Roy Keane.

  England imepangwa kundi moja na Hispania na Croatia kwenye michuano mipya ya UEFA PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Ireland Kaskazini ipo Kundi B3, na itacheza na Austria na Bosnia-Herzegovina wakati Scotland, iliyopo katika Ligi ya Tatu itacheza Israel na Albania. 
  Kocha mpya wa Wales, Giggs alikuwepo mjini Lausanne kuhudhuria droo hiyo na kujikuta anapangwanna Denmark. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ENGLAND YAPANGWA NA HISPANIA, CROATIA MICHUANO MIPYA UEFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top