• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 23, 2018

  UNAOWAONA NI MABOSI WA ARSENAL WANASHANGAA GARI LA AUBAMEYANG UJERUMANI

  Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis na Mkuu wa Usajili, Sven Mislintat wakilishangaa gari la Aubameyang aina ya Porsche Panamera PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  Porsche Panamera Turbo Techart 

  GHARAMA: Pauni 132,000
  UFUFUJI: 0-60mph in 3.9secs
  SPIDI: 182mph  
  MSAFARA wa Arsenal uliotumwa kwenda kushughulikia usajili Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund umejionea mfumo wa maisha ya kifahari ya mchezaji huyo.
  Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis na Mkuu wa Usajili, Sven Mislintat walipigwa picha mjini Dortmund wakiondoka kwenye gari kuingia kwenye mkutano na viongozi wenzake wa timu ya Ujerumani kuzungumzia uhamisho wa mchezaji huyo kumpelekea Ligi Kuu ya England.
  Na picha zimetokea zikiwaonyesha Gazidis na Mislintat wakizungumza na kulishangaa gari la kifahari aina ya Porsche Panamera Turbo Techart ambalo linamilikiwa na Aubameyang, mtu wanayetumaini kurejea naye Arsenal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UNAOWAONA NI MABOSI WA ARSENAL WANASHANGAA GARI LA AUBAMEYANG UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top