• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 29, 2018

  BEKI WA ZAMALEK ASAINI KWA MKOPO WEST BROMWICH ALBION

  KLABU ya West Bromwich Albion imemsajili beki Mmisri, Ali Gabr kwa mkopo kutoka Zamalek hadi mwishoni mwa msimu.
  Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imetangaza dili hilo katika tovuti yao rasmi, na imesema Gabr sasa ataungana na Mmisri mwenzake, Ahmed Hegazi katika safu ya ulinzi ya The Baggies.
  "Nipo hapa kuisaidia timu na kufanya kazi yangu. Nina furaha na nimevutiwa na kuwa hapa," alisema.
  Mkurugenzi wa Ufundi, Nick Hammond pia amesema: "NI mchezaji ambaye kwanza tulimuona katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ambako alikuwa anacheza na Ahmed.
  "Tuliendelea kumfuatilia tangu hapo na tukaona ni fursa nzuri kumchukua dirisha hili la usajili,".

  West Brom imemsajili beki Mmisri, Ali Gabr kwa mkopo kutoka Zamalek hadi mwishoni mwa msimu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  The Baggies inaweza kuendelea kusajili kabla ya dirisha kufungwa Jumatano baada ya klabu kuonyesha nia yake ya kuwachukua mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge na Nahodha wa Watford, Troy Deeney. 
  Alan Pardew ametenga dau la Pauni Milioni 18 kumsajili Deeney ambaye amepoteza nafasi kwa miezi kadhaa The Hornets na pia anamtaka kwa mkopo Sturridge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI WA ZAMALEK ASAINI KWA MKOPO WEST BROMWICH ALBION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top