• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 31, 2018

  ARSENAL YATHIBITISHA KWA 'BAHATI MBAYA' KUMSAJILI AUBAMEYANG

  KLABU ya Arsenal kwa 'bahati mbaya' imejikuta ikithibitisha kumsajili mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang baada ya kuposti kimakosa video ya kuthibitisha kuwasili kwake kwenye tovuti yao.
  Si kawaida kwa klabu kubwa kutumia mitandao ya kijamii kuposti video kutangaza wachezaji wake wapya iliyowasili.
  Lakini Arsenal ilifanya hivyo kimakosa jana baada ya kuweka video kwenye tovuti yake ikimuonyesha kocha wake, Arsene Wenger akithibitisha usajili wa Pauni Milioni 55 wa Aubameyang.
  Katika video hiyo fupi ya mahojiano na Wenger inasema; "Aubameyang ni mchezaji wa Arsenal, unaweza kuelezea furaha yako?'
  "Ndio, ni habari njema,"amejibu kocha wa Arsenal baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Swansea jana.

  Arsenal imethibitisha kwa 'bahati mbaya' kumsajili mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YATHIBITISHA KWA 'BAHATI MBAYA' KUMSAJILI AUBAMEYANG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top