• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 24, 2018

  MANCHESTER CITY YATANGULIA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND

  Mshambuliaji Sergio Aguero akishangilia na mchezaji mwenzake, Bernardo Silva baada ya kuifungia bao la pili dakika ya 49 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji, Bristol-City kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Carabao Cup Uwanja wa Ashton Gate usiku wa jana. Mabao mengine ya City yalifungwa na Leroy Sane dakika ya 43 na Kevin De Bruyne dakika ya 90 na ushei wakati mabao ya Bristol yamefungwa na Marlon Pack dakika ya 64 na Aiden Flint dakika ya 90 na ushei kabla ya bao la tatu la washindi. Man City inakwenda fainali ya Kombe la Ligi kwa ushindi wa jumla wa 5-3 baada ya kushinda 201 nyumbani kwenye mchezo wa kwanza na sasa itakutana na mshindi kati ya Arsenal na Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YATANGULIA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top