• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 28, 2018

  MOROCCO NA SUDAN ZATINGA NUSU FAINALI CHAN 2018

  WENYEJI, Morocco na Sudan wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi dhidi ya Namibia na Zambia usiku wa jana.
  Bao pekee la Saifeldin Bakhit dakika ya 32 lilitosha kuipa Sudan ushindi wa 1-0 dhidi ya Zambia Uwanja wa Marrakech, wakati mabao ya Ayoub El Kaabi dakika ya 37 na Salaheddine Saidi dakika ya 55 yalikamilisha ushindi wa 2-0 wa Simba wa Atlasi, Morocco dhidi ya  Namibia Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca.
  Robo Fainali za pili za CHAN ya 2018 zinafanyika leo, Nigeria wakiikaribisha Angola Uwanja wa Ibn Batouta Saa 1:30 usiku na Kongo wakiwa wenyeki wa Libya Uwanja wa Agadir Saa 4:30 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOROCCO NA SUDAN ZATINGA NUSU FAINALI CHAN 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top