• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 30, 2018

  AUBAMEYANG APANDA NDEGE DORTMUND KWENDA LONDON

  UHAMISHO wa Pierre-Emerick Aubameyang kwenda Arsenal kwa Pauni Milioni 55 kutoka Borussia Dortmund unakaribia baada ya mshambuliaji huyo kuonekana Uwanja wa Ndege wa Dortmund.  
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon, ambaye amekuwa akitakiwa na The Gunners kwa mwezi wote huu, alionekana akishusha mizigo yake kwenye Range Rover ya rangi ya dhahabu kabla ya kuingia ndani. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakwenda London kukamilisha uhamisho wake ambao utamfanya awe mchezaji ghali zaidi kihistoria ndani ya Arsenal.


  Pierre-Emerick Aubameyang ameonekana Uwanja wa Ndege wa Dortmund akisafiri kwenda London PICHA ZAIDI GONGA  

  Aubameyang alionekana akiwa na familia yake ambayo inatarajiwa kuungana naye katika safari hiyo.
  Dortmund imesema itamruhusu Aubameyang kuondoka mara tu itakapompata mbadala wake. Wanamtaka Batshuayi kwa mkopo na Chelsea wanaweza kukubaliana na hilo ikiwa watampata Giroud.
  Inaonekana kama Chelsea wanatafuta ujanja wa kuilazimisha Arsenal ipunguze bei ya Mfaransa huyo.
  Chelsea imetoa ofa ya Pauni Milioni 15 ambayo ni pungufu ya ada wanayotoa Arsenal, Pauni Milioni 30na kwa mkataba wa kiaka mitatu na nusu na mshahara wa Pauni 180,000 kwa wiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG APANDA NDEGE DORTMUND KWENDA LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top