• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 31, 2018

  REKODI YA ALEXIS SANCHEZ UWANJA WA WEMBLEY INATISHA

  MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez anatarajiwa kuichezea Manchester United mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya England itakapomenyana na Tottenham Hotspur leo Uwanja wa Wembley, London.
  Akitoka kucheza vizuri na kutoa pasi za mabao ya Marcus Rashford na Ander Herrera Man United ikishinda 4-0 dhidi ya Yeovil Town timu ya Ligi Daraja la Pili, Sanchez anahamia kwenye Ligi Kuu leo.
  Alexis alicheza mechi yake ya kwanza Uwanja huo wa Taifa miaka mitano iliyopita na tangu hapo amejiwekea rekodi nzuri ya kufunga mabao saba na kutoa pasi ya bao moja.

  Mshambuliaji Alexis Sanchez tayari amefunga mabao sana Uwanja wa Wembley kabla ya kujiunga Manchester PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mwezi Novemba mwaka 2013, aliweka kumbukumbu ya mwanzo nzuri baada ya kufunga mabnao yote mawili, Chile ikishinda 2-0 dhidi ya England.
  Pia alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza ya klabu kucheza Wembley, Arsenal ikishinda 2-1 dhidi ya Reading kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA Aprili mwaka 2015.
  Mwezi uliofuata, Alexis akafunga moja ya mabao ya mabao mazuri katika fainali ya Kombe la FA katika ushindi wa The Gunners wa 4-0 dhidi ya Aston Villa. 
  Baada ya kumsetia Theo Walcott kufunga bao la kwanza kipindi cha kwanza, akafunga bao lake muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili kutoka umbali wa mita 25 na kuwa Mchile wa pili tu kufunga kwemnye fainali ya michuano hiyo.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 pia alimaliza ukame wa Arsenal’ wa mataji ya Kombe la FA kwa muda mrefu msimu uliopita kwa kufunga bao lingine la dakika za lala salama kwenye Nusu Fainali akiisaidia timu yake kuifunga Manchester City 2-1 mwezi Aprili.
  Alexis kisha akafunga bao la mapema zaidi kwenye fainali ya Kombe la FA ambalo lilikuwa ni la kwanza baada ya sekunde 229 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea mwezi mmoja baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REKODI YA ALEXIS SANCHEZ UWANJA WA WEMBLEY INATISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top