• HABARI MPYA

  Wednesday, January 24, 2018

  WASUDAN KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA GENDARMERIE TNALE KOMBE LA SHIRIKISHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAAMUZI kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Soka Afrika (CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim ,mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Madir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai.
  Nahodha wa Simba SC, John Bocco (kushoto) ataiongoza timu yake dhidi ya Gendarmerie Tnale ya Djobouti Februari 21 Uwanja wa Taifa 

  Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21,2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda.
  Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo,mwamuzi msaidizi namba mbili Willy Habimana,mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WASUDAN KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA GENDARMERIE TNALE KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top