• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 30, 2018

  TUMBA ALIYEIBUKIA AZAM AKANG’ARA COASTAL NA MBEYA CITY ASAINI MIAKA MIWILI TIMU YA KENYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI Mtanzania, Tumba Lui Swedi amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu ya Wazito FC ya Kenya kutoka Maji Maji FC ya Songea.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Tumba amesema kwamba baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu anaona sasa ni wakati mwafaka kujaribu bahati yake nje ya mipaka.
  “Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujiunga na Wazito FC ya Ligi Kuu ya Kenya kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kumalizana na klabu yangu, Maji Maji ya Songea,”amesema Tumba.
  Tumba Swedi (kushoto) akikabidhiwa jezi ya Wazito FC baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili

  Kihistoria Tumba aliibukia katika akademi ya Azam FC kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2012 na baadaye kutolewa kwa mkopo Coastal Union ya Tanga.
  Hata hivyo, klabu ya Azam FC iliachana naye moja kwa moja mwaka 2013 naye akiunga na Mbeya City msimu uliofuata kabla zaidi Nyanda za Juu Kusini kwa kujiunga na Maji Maji.
  Wazito FC yenye maskani yake, Nairobi nchini Kenya inamilikiwa na watumishi wa Chuo Kikuu cha Nairobi na ndio imepanda Ligi Kuu ya Kenya kwa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TUMBA ALIYEIBUKIA AZAM AKANG’ARA COASTAL NA MBEYA CITY ASAINI MIAKA MIWILI TIMU YA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top