• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 31, 2018

  PERRE-EMERICK AUBAMEYANGA NI MCHEZAJI MPYA WA ASRENAL

  KLABU ya Arsenal imekamilisha uhamisho wa rekodi wa Pauni Milioni 56 wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani. 
  Dortmund imethibitisha kupitia kwenye akaunti yake ya Twitter leo, kabla ya Arsenal kutoa picha za Aubameyang akiwa na jezi yao na akiwa na kocha Arsene Wenger. 
  Anaweka rekodi ya mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu huyo, Pauni 180,000 kwa wiki baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu.
  Kusajiliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutafungua milango ya mshambuliaji wa Arsenal, Mfaransa Olivier Giroud kuhamia Chelsea ambao nao watamruhusu Michy Batshuayi kwenda Dortmund kuziba pengo la Aubameyang. 

  Arsene Wenger akipeana mikono Pierre-Emerick Aubameyang baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa Pauni Milioni 56 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PERRE-EMERICK AUBAMEYANGA NI MCHEZAJI MPYA WA ASRENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top