• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 29, 2018

  LIBYA, NIGERIA ZATINGA NUSU FAINALI CHAN, KONGO NA ANGOLA NJE

  TIMU ya taifa ya Libya jana imekwenda fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa penalti 5-3 dhidi ya Kongo kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 kwenye mchezo wa Robo Fainali Uwanja wa Agadir nchini Morocco.
  Katika mchezo huo , Saleh Taher alitangulia kuifungia Libya bao la kuongoza dakika ya 15, kabla ya Junior Makiesse kuwasawazishia Wakongo dakika ya 37.
  Kipa wa Kongo, Barel Mouko ndiye aliyewaondoa mashindanoni wenzake baada ya kipiga juu mkwaju wake wa penalti, hivyo mabingwa wa 2014 kuwafuata wenyeji, Morocco katika Nusu Fainali inayotarajiwa kuwa kali.
  Moftah Taktak, Ramadan, Alaqoub, Ahmed Almaghasi na Sand Masaud walifunga penalti za Libya wakati Francouer Kibamba, Mboungou na Varel Rozan walifunga za Kongo.
  Mapema kwenye mchezo huo, Mouko aliisaidia mno timu yake kwa kuokoa mno hatari nyingi zilizopelekwa na Libya langoni mwake.
  Katika mchezo mwingine wa Robo Fainali jana, Mtokea benchi Gabriel Okechukwu aliifungia Nigeria bao la ushindi dakika ya 108 ikitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Angola mjini Tangiers hivyo kwenda Nusu Fainali.
  Angola ilitangulia kwa bao la Vladimir Va dakika ya 55 baada ya makosa ya Emeka Atuloma na mpira ukamkuta yeye hivyo kumtungua kipa Ikechukwu Ezenwa, kabla ya Anthony Okpotu kuisawazishia Nigeria dakika ya 90 na ushei. 
  Okechukwu akafunga bao la ushindi kwenye dakika 30 za nuongeza na sasa Nigeria itakutana na Sudan katika Nusu Fainali Jumatano mjini Marrakech.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIBYA, NIGERIA ZATINGA NUSU FAINALI CHAN, KONGO NA ANGOLA NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top