• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 25, 2018

  MOURINHO ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED HADI 2020

  KOCHA Mreno, Jose Mourinho amejitia kitanzi katika klabu ya Manchester United baada ya kusaini mkataba wa ytakaomuweka hadi angalau mwaka 2020 wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja.
  Akiuzungumzia mkataba wake mpya, Mourinho amesema kwamba: "Tayari nimepewa heshima na ninajivunia kuwa kocha wa Manchester United,". 
  "Ningependa kutoa shukrani kubwa kwa wamiliki na Woodward kwa kutambua kazi yangu ngumu na kuithamini. Nafurahi wanahisi na wanaamini mimi ni kocha sahihi kwa klabu hii kubwa kwa kipindi hicho kijacho,".


  Jose Mourinho akipeana mikono na Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward baada ya kusaini mkataba mpya hadi mwaka 2020 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  "Tumeweka kiwango cha juu sana - kushinda mataji matatu katika msimu mmoja - lakini hivyo ni viwango ninatarajia timu zangu zilenge kuvifikia. Tunatengeneza mazingira ya mafanikio zaidi kwa mustakabali wa Manchester United.
  "Shukrani zangu ziende kwa kadhalika ziende kwa wasaidizi wangu na kwa wachezaji wangu; bila huruma yao na urafiki hili lisingewezana. Nawapenda wachezaji wangu na ni faraja kujua tunakwenda kuwa pamoja angalau kwa misimu mingine mitatu,".
  "Na siwezi kumaliza bila kuwashukuru mashabiki kwa sapoti yao na kunifanya mimi nijisikie nipo nyumbani haraka. Narudia, kuwa kocha wa Manchester United ni heshima kila siku na nina furaswa haswa,"amesema Mourinho.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED HADI 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top