• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 25, 2018

  ANGOLA YAFUNGA MLANGO WA ROBO FAINALI CHAN 2018

  TIMU ya taifa ya Angola imekamilisha orodha ya timu nane za Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya sare ya 0-0 na Kongo katika mchezo wa mwisho wa Kundi D usiku wa jana Uwanja wa Agadir nchini Morocco.  
  Matokeo hayo yanamaanisha, Angola inamaliza nafasi ya pili Kundi D kwa pointi zake tano, nyuma ya Kongo yenye pointi saba sasa na zote zinakwenda Robo Fainali. 
  Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi D jana, Burkina Faso ilitoa sare ya 1-1 Cameroon Uwanja wa Ibn Batouta na zote zimetolewa.
  Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Morocco, Sudan kutoka Kundi A, Zambia, Namibia Kundi B, Nigeria na Libya kutoka Kundi C.
  Nusu zitakuwa ni Morocco na Namibia Jumamosi Saa 10:30 jioni Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca na Zambia na Sudan Saa 1:30 usiku Uwanja wa Marrakech, Marrakech, wakati Jumapilki Nigeria itamenyana na Angola Saa 10:30 Uwanja wa Ibn Batouta, Tangier na Kongo na Libya Saa 1:30 usiku Uwanja wa Adrar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ANGOLA YAFUNGA MLANGO WA ROBO FAINALI CHAN 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top