• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 31, 2018

  OZIL AKUBALI KUJITIA PINGU ARSENAL KWA MIAKA MITATU MINGINE

  KIUNGO mshambuliaji Mesut Ozil amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Arsenal kwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki.
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, Ozil amesaini mkataba mwingine wa miaka mitatu kuendelea kuichezea Arsenal. 
  Hiyo inamaanisha kwamba zile tetesi za kwamba Mjerumani huyo ataondoka London zimezimwa. 
  Tangu mwezi Desemba mwaka jana ilikwishajulikana kwamba The Gunners wanahangaika kumshawishi Ozil asaini mkataba mpya.

  Mesut Ozil amekubali kusaini mkataba wa kuendelea kuichezea Arsenal kwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OZIL AKUBALI KUJITIA PINGU ARSENAL KWA MIAKA MITATU MINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top