• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 29, 2018

  AMIR KHAN KUREJEA ULINGONI BAADA YA MIAKA MIWILI

  BONDIA Amir Khan atarejea ulingoni baada ya miaka miwili kwa kupambana na Phil Lo Greco Aprili 21 ukumbi wa Echo Arena mjini Liverpool.
  Pambano hilo ni mwanzo wa mkataba wa mapambano matatu baina ya Khan na promota Matchroom Boxing na la kwanza tangu apigwe kwa Knockout (KO) na bingwa wa WBC uzito wa Middle wakati huo, Saul 'Canelo' Alvarez Mei 2016.
  Khan atashusha uzito atakapopambana na Lo Greco katika pambano la uzito wa Welter. 
  Lo Greco ameshinda mapambano 28 kati ya 31 ya ngumi za kulipwa aliyocheza na amewahi kupigana na bingwa wa sasa wa IBF, Errol Spence Jr na Shawn Porter aliyewahi kuushikilia mkanda huo, ambao wote walimpiga Mcanada huyo.

  Amir Khan atarejea ulingoni baada ya miaka miwili kwa pambano litakalofanyika mjini Liverpool Aprili mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AMIR KHAN KUREJEA ULINGONI BAADA YA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top