• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 25, 2018

  REAL MADRID YATOLEWA NA LEGANES KOMBE LA MFALME

  Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos akiwahamasisha wachezaji wenzake wakati wa mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey usiku wa jana timu yake ikifungwa 2-1 na Leganes Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid. Mabao ya Leganes yalifungwa na Javier Eraso dakika ya na Gabriel Appelt Pires dakika ya 55 wakati la Real iliyowakosa nyota wake, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale lilifungwa na Karim Benzema dakika ya 47.
  Real ya kocha Mfaransa, Zinadine Zidane imetolewa kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2, kufuatia enhyewe kushinda 1-0 ugenini kwenye mchezo wa kwanza PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID YATOLEWA NA LEGANES KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top