• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 24, 2018

  MASCHERANO ANAAGWA LEO BARCELONA ANATIMKIA CHINA

  Barcelona imethibitisha Javier Mascherano anaondoka katika klabu hiyo na ataagwa leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  CRUFF NA JEZI NAMBA 14

  Johan Cruyff alikuwa maarufu kwa jezi namba 14. 
  Wakati hakuwahi kuvaa jezi hiyo alipokuwa Barcelona, aliivaa tu kwa klabu yake nyingine, Ajax na timu yake ya taifa ya Uholanzi — tofauti na agizo la Chama cha Soka Uholanzi kutaka timu ifuate utaratibu wa namba moja hadi 11 uwanjani. 
  Ajax iliistaafisha jezi hiyo moja kwa moja mwaka 2007 kwa heshima ya Cruyff kutokana na mchango wake katika klabu.  
  TIMU ya Barcelona imethibitisha kwamba Javier Mascherano ataondoka kwenye klabu hiyo, kwani kiungo huyo Muargentina anahamia Ligi Kuu ya China.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa akihusishwa na kuhamia Hebei China Fortune mweszi huu na kuhitimisha miaka saba na nusu ya kutumika Nou Camp.
  Na klabu yake imethibitisha kwa taarifa iliyoitoa jana Mascherano ataagwa kwa tafrija maalum.
  Taarifa imesema: "Javier Mascherano anaondoka FC Barcelona baada ya misimu saba na nusu. 
  "Muargentina huyo ataagwa kwa tafrija maalum klabunu Jumatano asubuhi Auditori 1899, katika sherehe ambayo itarushwa moja kwa moja kwenye tovuti ya klabu,".
  'Itahudhuriwa na Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu na wachezaji wa kikosi cha kwanza,".
  Mascherano ameshinda mataji manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wake akiwa Barcelona. 
  Alijunga na Barca akitokea Liverpool mwaka 2010, na anaondoka wakati klabu inapokea ugeni mwingine kutoka Anfield kufuatia kusajiliwa kwa Philippe Coutinho ambaye bado hajapatiwa namba ya jezi. 
  The Blaugrana wanaweza kumpa jezi namba 14 Coutinho ambayo inaachwa wazi na Mascherano, namba ambayo ilitumiwa na gwiji mwingine Barcelona.
  Johan Cruyff alikuwa anavaa namba hiyo akiichezea timu yake ya taifa ya Uholanzi tu, wakati hakuwahi kuvaa namba 14 akiwa Barca.
  Mbrazil huyo hajawahi kupangiwa namba ya jezi tangu akamilishe uhamisho wake wa Pauni Milioni 145 mapema mwezi huu.
  Ilifikiriwa atapewa jezi namba saba baada ya Arda Turan kuhamia Istanbul Basaksehir kwa mkopo mapema mwezi huu, lakini taarifa zinasema hiyo imehifadhiwa kwa ajili ya Antoine Griezmann, anayetarajiwa kujiunga na Barcelona mwishoni mwa msimu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASCHERANO ANAAGWA LEO BARCELONA ANATIMKIA CHINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top