• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 25, 2018

  XHAKA AIPELEKA ARSENAL FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND

  Granit Xhaka (kulia) akishangilia na Alexandre Lacazette (kushoto) baada ya kuifungia bao la pili Arsenal dakika ya 60 ikishinda 2-1 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge, London. Chelsea ilitangulia kwa bao la Eden Hazard dakika ya saba, kabla ya Arsenal kusawazisha kwa bao la kujifunga lao Antonio Rudiger dakika ya 12, kufuatia kubabatizwa na mpira uliopigwa na Nacho Monreal. Baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Stamford Bridge, Arsenal sasa inakwenda Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup ambako itakutana na Manchester City iliyoitoa Bristol City juzi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: XHAKA AIPELEKA ARSENAL FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top