• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 24, 2018

  WAHABESHI KUCHEZESHA YANGA NA SAINT LOUIS FC LIGI YA MABINGWA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Africa (CAF) limetaja waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza na mchezo wa pili wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Saint Louis FC ya Shelisheli.
  Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 10, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea nchini Namibia.
  Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi.
  Mechi ya kwanza kati ya Yanga na Saint Louis FC ya Shelisheli itachezeshwa na marefa kutoka Ethiopia

  Mechi ya pili itakayochezwa Seychelles kati ya Februari 20 na 21,2018 itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar na kamishna atatoka Mauritius.
  Mwamuzi wa kati atakuwa Andofetra Avombitana Rakotojaona akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina na mwamuzi msaidizi namba mbili Pierre Jean Eric Andrivoavonjy na mwamuzi wa akiba Hamada el Moussa Nampiandraza,kamishna wa mchezo huo Ahmad Nazeer Hossen Bowud.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAHABESHI KUCHEZESHA YANGA NA SAINT LOUIS FC LIGI YA MABINGWA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top