• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 23, 2018

  PICHA INAYODHIHIRISHA SANCHEZ NI MANCHESTER UNITED DAMU

  Sanchez akiwa na rafiki yake amevalia jaketi lenye nembe la Mashetani hao Wekundu PICHA ZAIDI GONGA HAPA   MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez amesema kwamba alikuwa ana ndoto ya kuchezea Manchester United tangu akiwa mdogo hivyo amefurahi mno kutua Old Trafford kwa Mashetani Wekundu. 
  Picha inayomuonyesha Sanchez mdogo akiwa amevaa jaketi la Manchester United imesambaa kwenye mitandao ya kijamii saa chache baada ya kukamilisha uhamisho wake. 
  Mtumia Twitter kwa jina la Poets Corner ametweet picha ya Sanchez akiwa na rafiki yake amevalia jaketi lenye nembe la Mashetani hao Wekundu.
  Katika mahojiano yake ya kwanza na vyombo vya habari baada ya kutua United, Sanchez amesema kwamba wakati wote alikuwa anaipenda klabu hiyo na pia alizungumza na kocha wa zamani, Sir Alex Ferguson juu ya uwezekano wa kucheza chini ya kocha huyo gwiji.  
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amezungumzia kuwasili kwake Old Trafford baada ya kubadilishwa na Henrikh Mkhitaryan: "Tangu nikiwa mdogo, nilikuwa ninasema wakati wote ndoto zangu zilikuwa ni kuchezea Manchester United, na sisemi kwa sababu nipo hapa sasa na leo yametimia. 
  Sanchez alitarajiwa kuhamia Manchester City kwenda kuungana tena na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola aliyefanya naye kazi Barcelona. 
  Hata hivyo, Man City ilishindwa kumchukua kwa kuhofia kukiuka sera zake za ulipaji mishahara, ambayo ikawapa mwanya mahasimu wao, United kumnyakua nyota huyo wa Chile. 
  Sanchez aliyetarajiwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya kwa mara ya kwanza leo, anaweza kuanza kuichezea United dhidi ya Yeovil Town Ijumaa katika Kombe la FA. 
  Mchezaji huyo mpya kusajiliwa na Jose Mourinho yuko huru kuichezea United katika Kombe la FA baada ya kutoichezea Arsenal ikifungwa 4-2 na Nottingham Forest katika Raundi ya Tatu.
  Ikiwa Sanchez hatacheza Ijumaa, basi ataanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Tottenham Januari 31.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PICHA INAYODHIHIRISHA SANCHEZ NI MANCHESTER UNITED DAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top