• HABARI MPYA

    Tuesday, January 23, 2018

    ISMAIL SUMA ALIYEDAKIA YANGA, SIMBA AFARIKI DUNIA BURUNDI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ismail Suma aliyedakia klabu za Simba na Yanga za Dar es Salaam amefariki dunia leo mjini Bumbura, Burundi.
    Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, Juma Athumani Salum ni kwamba Suma amefariki leo asubuhi mjini Bujumbura baada ya kusumbuliwa na maradhi ya ini na figo kwa muda mrefu.
    Suma alikuwa anacheza nchini Burundi alikokwenda akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako alicheza pia akitokea nyumbani Tanzania.
    Ismail Suma (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Yanga mwaka 2000, Ally Mayay, Iddi Moshi na Stephen Nyenge
    Mpango wa awali ulikuwa ni kuurejesha mwili wa marehemu kwa mazishi kwao mkoani Tabora, lakini imeshindikana kutokana na wafiwa kutokuwa na fedha za kutosha gharama za kusafirisha maiti.
    Na kwa sababu hiyo wamepanga kumzika ndugu yao huyo huko huko mjini Bujumbura jioni ya leo.
    Suma aliibukia Kariakoo United ya Lindi mwaka 1998 na akadaka hadi mwaka 2000 alipohamia Yanga SC kabla ya baadaye kuchezea timu nyingine kadhaa, ikiwemo Simba SC na African Lyon wakati bado inaitwa Mbagala Market ingawa ilivyopanda Ligi Kuu akaondoka.
    Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ismail Suma. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ISMAIL SUMA ALIYEDAKIA YANGA, SIMBA AFARIKI DUNIA BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top