• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 30, 2018

  PETER APIGA HAT TRICK AZAM FC YAITANDIKA SHUPAVU 5-0 ASFC MOROGORO

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  AZAM FC imetinga hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Shupavu FC mchana wa leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Chipukizi Paul Peter ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo wa leo baada ya kufunga mabao matatu peke yake katika dakika za 52, 77 na 88 baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mbaraka Yussuf Abeid. 
  Mabao mengine ya Azam FC leo yamefungwa na chipukizi wengine, Yahya Zayed dakika ya 45 na Iddi Kipagwile dakika ya 45 na Iddi Kipagwile dakika ya 45 na ushei.
  Mechi zaidi za Azam Sports Federations Cup zinachezwa jioni ya leo, Yanga SC wakimenyana na Ihefu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Paul Peter ameendeleza makali yake ya kufunga mabao leo, akipiga hat trick Azam FC ikishinda 5-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PETER APIGA HAT TRICK AZAM FC YAITANDIKA SHUPAVU 5-0 ASFC MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top