• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 31, 2018

  GIROUD AKAMILISHA UHAMISHO WAKE CHELSEA KUTOKA ARSENAL

  KLABU ya Chelsea imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Oliver Giroud kutoka Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 18.
  The Gunners wamekubali kumuuza Giroud kwa mahasimu wao wa London baada ya kukamilisha usajili wa rekodi wa klabu yao wa Pauni Milioni 56 wa Pierre-Emerick Aubameyang. 
  Dortmund ilikuwa tayari kumuuza Aubameyang mara tu itakampopata mbadala wake na kwa kumpata mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi, ambaye amefanyiwa vipimo vya afya nchini Ujerumani leo asubuhi dili limekamilika. 
  Klabu hizo mbili bado hazijatangaza uhamisho wa Giroud, lakini naye pia amekamilisha vipimo vya afya mjini London.
  Olivier Giroud amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 18 kwenda Chelsea kutoka Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Kusajiliwa kwa Giroud kunazima mpango wa Chelsea kuendelea kusaka mshambuliaji Januari hii, baada ya awali klabu hiyo kuwa katika mpango wa kuwasajili Edin Dzeko wa Roma, Andy Carroll wa West Ham na hata mkongwe wa umri wa miaka 37 wa Stoke City, Peter Crouch. 
  Giroud mwenye umri wa miaka 31 raia wa Ufaransa, aliyecheza kwa miaka mitano na nusu Arsenal, aliichezea Gunners jana akiingia dakika 15 za mwisho ikichapwa 3-1 na Swansea City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GIROUD AKAMILISHA UHAMISHO WAKE CHELSEA KUTOKA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top