• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 31, 2018

  MAN UNITED YAMUONGEZEA MKATABA JUAN MATA HADI 2019

  KLABU ya Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja Juan Mata ambao utamalizika Juni 2019. Kocha Mreno, Jose Mourinho amezungumza na Mspaniola huyo, Mata mara kadhaa wiki za karibuni na akafanya hivyo tena Jumatatu, kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mechi na Tottenham Hotspur.
  Baada ya kuthibitisha kwamba klabu imemuongezea mkataba kiungo huyo, Mourinho alisema: “Mata ni muhimu sana. Nilipowasili hapa mwaka mmoja na nusu uliopita, [walisema], ‘Mata yuko matatizoni, kwenye matatizo, kwenye matatizo’, na sasa ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja. Kwa mchezaji muhimu kwangu; mchezaji muhimu kwa klabu; mchezaji muhimu kwa wachezaji wengine."

  Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja Juan Mata hadi Juni 2019 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kinachofuata kwa Mata na wachezaji wenzake ni safari ya Uwanja wa Wembley Jijii kwa ajili ya mechi na wenyeji, Tottenham Hotspur leo Man United wakisaka ushindi wa sita mfululizo kwenye mashindano yote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAMUONGEZEA MKATABA JUAN MATA HADI 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top