// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SENEGAL WAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUIPIGA 2-0 BAFANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SENEGAL WAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUIPIGA 2-0 BAFANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 11, 2017

    SENEGAL WAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUIPIGA 2-0 BAFANA

    TIMU ya soka ya taifa ya Senegal imekata tiketi ya fainali za kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Afrika Kusini Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane jana.
    Mabao ya Senegal yalifungwa na mshambuliaji wa West Ham, Diafra Sakho dakika ya 12 na Thamsanqa Mkhize aliyejifunga dakika ya 38.
    Ikumbukwe huo ulikuwa mchezo wa marudio, baada ya ushindi wa 2-1 wa Bafana Bafana Novemba 12 mwaka jana kutenguliwa na kuamriwa mechi irudiwe, kufuatia refa Joseph Lamptey kufungiwa maisha na Mahakama ya Usuluhishi (CAS). 
    Wachezaji wa Senegal wakisherehekea baada ya ushindi wa jana unaowapeleka Kombe la Dunia mwakani nchini Russia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    FIFA ilimkuta na hatia Lamptey ya kupanga matokeo ili kuibeba Afrika Kusini.
    Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane ndiye aliyetoa pasi ya bao lililofungwa na Sakho na Senegal inakuwa nchi ya tatu ya Afrika kujihakikishia tiketi ya Urusi mwakani, baada ya Misri na Nigeria kuwa za kwanza kufuzu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SENEGAL WAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUIPIGA 2-0 BAFANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top