• HABARI MPYA

  Monday, November 27, 2017

  LWANDAMINA AWAPA ‘OFF’ WACHEZAJI WOTE YANGA SIKU SABA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina ametoa wiki moja ya mapumziko kwa wachezaji wake kufuatia mechi 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu ikiwa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam.  
  Taarifa ya Yanga SC jioni ya leo imesema kwamba kocha Lwandamina ametoa siku saba za mapumziko kwa wachezaji wake kuanzia leo Jumatatu kikosi kitarejea tena mazoezini Jumatatu ijayo.
  Yanga inakwenda mapumzikoni ikitoka kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu juzi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kocha Mzambia wa Yanga, George Lwandamina ametoa wiki moja ya mapumziko kwa wachezaji wake 

  Katika mchezo huo uliochezeshwa na Shomary Lawi wa Kigoma aliyesaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, Prisons walitangulia kwa  bao la Eliuter Mpepo dakika ya tisa akitumia makosa ya mabeki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ waliochanganyana na kipa wao, Mcameroon, Youth Rostande na kushindwa kuokoa.
  Prisons walipata pigo dakika ya 36 baada ya mchezaji wake, Lambert Sibiyanka kutolewa kwa kadinyekundu na refa Lawi kufuatia kumpiga kiwiko beki wa Yanga, Juma Abdul.
  Yanga walitumia mwanya huo kuongeza mashambulizi kusaka bao la kusawazisha na wakafanikiwa kupata bao dakika ya 41, lililofungwa na kiungo Raphael Daudi aliyemalizia krosi ya mshambuliaji Ibrahim Ajib.
  Kwa sare hiyo, Yanga inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 11, ikizidiwa pointi mbili mbili na Simba na na moja na Azam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWAPA ‘OFF’ WACHEZAJI WOTE YANGA SIKU SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top