• HABARI MPYA

  Wednesday, November 22, 2017

  KOCHA WA SEVILLA ANASUMBULIWA NA SARATANI YA KIBOFU

  KOCHA wa Sevilla ya Hispania, Eduardo Berizzo amegundulika ana tatizo la saratani la kibofu, klabu hiyo ya Hispania imethibitisha leo asubuhi.
  Uthibitisho wa kocha huyo Muargentina mwenye umri wa miaka 48 kuwa na tatizo hilo ulitolewa wakati wa mapumziko timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 3-0 mbele ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.
  Taarifa iliyotolrwa na klabu hiyo imesema: “Taarifa ya idara ya tiba ya Sevilla FC ni kwamba kocha wa timu ya kwanza, Eduardo Berizzo amekutwa na tatizo ya saratani ya kibofu.
  Eduardo Berizzo amegundulika ana tatizo la saratani la kibofu, klabu hiyo ya Hispania imethibitisha leo asubuhi

  Vipimo zaidi vitaamua hatua inayofuata ya matibabu. Sevilla FC inataka kuonyesha sapoti kamili kwa kocha wake kwa sasa na inamtakia kupona haraka,”.
  Guido Pizarro aliifungia Sevilla bao la tatu la kusawazisha dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida katika mechi ya jana na wachezaji wote wakamkimbilia kocha Berizzo kushangilia naye.  
  Inafahamika Muargentina huyo ambaye aliisaidia Celta Vigo kufika Nusu Fainali ya Europa League msimu uliopita, atakwenda kufanyiwa matibabu baadaye.
  Walikuwa nyuma kwa mabao matatu baada ya nusu saa ambayo yalifungwa na Roberto Firmino mawili na Sadio Mane moja, lakini mabao mawili ya Yassim Ben Yedder yakawazindua kabla ya Pizarro kukamilisha sare dakika ya mwisho. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA SEVILLA ANASUMBULIWA NA SARATANI YA KIBOFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top