• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 22, 2017

  YAKUBU ASTAAFU SOKA BAADA YA KUTEMWA NA TIMU YA DARAJA LA TATU

  MSHAMBULIAJI wa zamani  wa Portsmouth na Everton za England, Yakubu Aiyegbeni amestaafu soka akiwa anatimiza miaka 35 tangu azaliwe.
  Yakubu, ambaye pia alichezea Middlesbrough na Blackburn Rovers, amecheza jumla ya mechi 250 za Ligi Kuu ya England na kufunga mabao 96 enzi zake katika miaka yake 20 ya kucheza.
  Ameichezea pia mechi tatu timu ya Daraja la Tatu, Coventry City mwaka huu kabla ya kutemwa. "Ningependa kutangaza rasmi kustaafu soka ya kulipwa leo,"amesema Yakubu leo.
  Mshambuliaji huyo mwenye nguvu, amefanya mabao 21 katika mechi 57 alizoichezea timu ya taifa ya Nigeria, zikiwemo fainali nne za Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na Kombe la Dunia 2010.
  Yakubu ni mfungaji wa tatu wa muda wote wa timu ya taifa kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Nigeria kwa mabao yake 21, akiwafuatia Segun Odegbami mabao 22 na Rashid Yekini mabao 37.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAKUBU ASTAAFU SOKA BAADA YA KUTEMWA NA TIMU YA DARAJA LA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top