• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2017

  MAVUGO MRUNDI PEKEE ANAYECHEZA TANZANIA ALIYEITWA KIKOSI CHA INT’HAMBA MURUGAMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Simba, Laudit Mavugo ni mchezaji pekee anayecheza Tanzania aliyeitwa kwenye kikosi cha Burundi ‘Int’hamba Murugamba’ kwa ajili ya michuano ya CECAFA Challenge inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu nchini Kenya. 
  Wengine wote wanaocheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakiwemo kiungo Yussuf Ndikumana wa Mbao FC ya Mwanza na mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga ya Dar es Salaam hawajaitwa.
  Kikosi kamili cha Burundi ni; Nahimana Jonathan (Vital’o FC), Rukundo Onesime (Messager Ngozi), Arakaza Mc Arthur (Kakamega - Kenya), Harerimana Rachid Leon (LLB-S4A), Nahimana Steve (Aigle Noir), Ndikumana Trésor (Amagaju), Nshimirimana David (Mukura Victory - Rwanda), Ndoriyobija Eric (LLB-S4A).
  Laudit Mavugo (kushoto) ni Mrundi pekee anayecheza Tanzania aliyeitwa kwenye kikosi cha Int’hamba Murugamba 

  Wengine ni  Moussa Omar (Bugesera), Duhayindavyi Gaël (Mukura - Rwanda), Urasenga Cédric Dany (Messager Ngozi), Ndayishimiye Yussuf Nyange (Aigle Noir), Moussa Mossi (LLB-S4A), Abdoul Fiston, Mavugo Laudit (Simba), Harerimana Moussa Hafiz (LLB-S4A), Kwizera Pierre (Rayon Sport - Rwanda), Hussein Shabani (Amagaju), Shaka Bienvenue (Aigle Noir) na Nahimana Shasiri (Rayon Sport).
  Burundi imepangwa Kundi B pamoja na mabingwa watetezi, Uganda, Zimbabwe, Ethiopia na Sudan Kusini, wakati Kundi A lina timu za Tanzania Bara, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya.
  Burundi itaanza na Ethiopia Desemba 4, kabla ya kumenyana na Uganda Desemba 6, Zimbabwe Desemba 8 na kukamilisha mechi zake za makundi kwa kumenyana na Sudan Kusini Desemba 10.
  Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAVUGO MRUNDI PEKEE ANAYECHEZA TANZANIA ALIYEITWA KIKOSI CHA INT’HAMBA MURUGAMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top