• HABARI MPYA

  Saturday, November 25, 2017

  NDEMLA AFUZU MAJARIBIO SWEDEN, ‘MAMILIONI’ YANUKIA SIMBA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba imesema kiungo wake, Said Hamis Juma, maarufu Said Ndemla amefanikiwa kufuzu majaribio yake ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden. 
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari kwamba Eskilstuna wamesema wameridhishwa na uwezo wa Ndemla na wako tayari kumnunua.
  “Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja. Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko,” amesema Manara. 
  Said Ndemla amefuzu majaribio klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden 

  Msemaji huyo wa Simba amesema kwamba klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi. “Na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla,”. 
  Katika hatua nyingine, Manara amesema kwamba kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi . makao makuu ya klabu, Msimbazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 4:00 asubuhi7. Amesema mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa Desemba 3, mwaka huu
  Wakati huo huo: Hajji Manara amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuishangilia timu yao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Lipuli ya Iringa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDEMLA AFUZU MAJARIBIO SWEDEN, ‘MAMILIONI’ YANUKIA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top