• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 25, 2017

  LIGI KUU YA WANAWAKE KUFUNGULIWA KESHO ARUSHA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSIMU wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake unatarajiwa kufunguliwa kesho kwa hafla itakayofanyika kwenye kituo cha Arusha, ambako kutakuwa na mechi za Kundi B.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema kwamba kikao cha pamoja baina ya viongozi wa timu za kituo cha Arusha kuhusu taratibu kimefanyika leo Arusha.
  Taarifa hiyo imesema timu zote za Kundi B zimeweka kambi Shule ya Trust St.Patrick.
  Kundi B linaundwa na timu za Alliancea, Marsh Academy za ya Mwanza, Panama ya Iringa, Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens ya Singida.
  Kundi A linaundwa na timu za Simba Queens, mabingwa watetezi, Mlandizi Queens, Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen zote za Dar es Salaam na Fair Play ya Tanga.
  Fungua dimba kwa Kituo cha Dar es Salaam, mabingwa watetezi wa taji hilo, Mlandizi Queens itacheza na JKT Queens katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
  Katika kundi hilo la A, mechi nyingine zitakuwa siku inayofuata Novemba 27, mwaka huu kati ya Mburahati Queens na Evergreen saaa 8.00 mchana wakati Fair Play ya Tanga itacheza na Simba Queens saa 10.00 jioni.
  Jijini Arusha, Panama ya Iringa itafungua dimba na Alliance Queens ya Mwanza huku siku ya pili Novemba 27, mwaka huu Baobab Queens itacheza na Marsh Academy saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni Majengo Queens itapambana na Sisterz ya Kigoma.
  Timu hizo zitapambana katika vituo hadi Desemba 12, mwaka huu kabla ya kutoa jumla ya timu nane kwa maana ya nne kutoka kila kundi. Timu hizo nane zitapambana katika hatua ya Nane Bora ya Ligi hiyo kuelekea ubingwa. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI KUU YA WANAWAKE KUFUNGULIWA KESHO ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top