• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 27, 2017

  AZAM FC NA MTIBWA SUGAR HAKUNA MBABE, SARE 1-1 CHAMAZI

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeshindwa kuitoa juu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanaamisha Azam FC inajiongezea pointi moja na kufikisha 23 sawa na Simba baada ya timu zote kucheza mechi 11, lakini Wekundu wa Msimbazi wanaendelea kuongoza kwa wastani wao mzuri wa mabao.
  Mtibwa Sugar wao baada ya kujiongezea pointi moja leo, wanafikisha 18 pia baada ya mechi 11 na kuendelea kukamata nafasi ya tano, nyuma ya Singida United yenye pointi 20 na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 21.  
  Katika mchezo wa leo, baada ya dakika 45 tasa za kipindi cha kwanza, Azam walitangulia kupata bao kipindi cha pili lililofungwa na winga Mghana, Enock Ata Agyei dakika ya 55 akimalizia pasi safi ya mshambuliaji Mbaraka Yusuph.
  Mtibwa Sugar wakafanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Kelvin Kiduku dakika ya 75 kwa shuti la mpira wa adhabu zikiwa ni dakika tano tu tangu aingie kucbhukua nafasi ya Salum kihimbwa dakika ya 70.   
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa, Razack Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed, Agrey Morris, Salmin Hoza, Frank Domayo/Idd Kipangwile dk63, Salum Aboubakar, Mbaraka Yusupu, Yahya Zayd na Enock Atta Agyei/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk83.
  Mtibwa, Benedict Tinoco, Rogers Gabriel, Issa Rashid, Dickson Daud, Cassian Ponera, Shaaban Nditi, Ally Makalani, Mohamed Issa, Stamili Mbonde/Haroun Chanongo dk84, Hassan Dilunga na Salum Kihimbwa/Kelvin Kiduku dk70.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC NA MTIBWA SUGAR HAKUNA MBABE, SARE 1-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top