• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 26, 2017

  MSUVAAA….UTAMTAKA! AFUNGA TENA DIFAA EL JADIDA IKISHINDA 3-0 LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva leo amefungua biashara nzuri timu yake Difaa Hassan El – Jadida ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Racing De Casablanca Uwanja wa Pere-Jego mjini Casablanca.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama  Botola, Msuva alifunga bao la kwanza dakika ya nane na baada ya hapo timu yake ikafunguka na kupata mabao mawili zaidi.
  Ayoub Nanah alifunga bao la pili dakika ya 37 kabla ya Bilal El Magri kushindilia msumari wa moto kwenye kidonda cha Racing De Casablanca dakika ya 69.
  Simon Msuva akikimbia kushangilia baada ya kufunga leo 
  Simon Msuva akinyoosha mikono juu kumshukuru Mungu baada ya kufunga
  Simon Msuva (wa pili kushotio) mstari wa mbele kwenye kikosi cha kwanza cha Difaa Hassan El- Jadida leo

  Baada ya kazi nzuri katika mchezo wa leo, winga wa zamani wa Yanga, Msuva akampisha Mario Bernard kipindi cha pili, wakati El Magri naye alimpisha Zakaria Alyoud na Nanah akampisha Youness Hawassi.
  Ushindi huo katika mechi ya saba ya msimu wa Ligi, unaifanya DHJ ifikishe pointi 14 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 16 za mechi tisa. 
  Kikosi Cha Difaa Hassan El – Jadida Kilikuwa; Yahia El Filali, Youssef Aguerdoum, Marouane Hadhoudi, Anouar Jayid, Tarik Astati, Mohammed Ali Bemaammer, Adil El Hasnaoui, Ayoub Nanah/Youness Hawassi, Bilal El Magri/ Zakaria Alyoud, Adnane El Ouardy na Simon Msuva/Mario Bernard.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVAAA….UTAMTAKA! AFUNGA TENA DIFAA EL JADIDA IKISHINDA 3-0 LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top