• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 27, 2017

  MWAKYEMBE AWATAKA WACHEZAJI LIGI YA WANAWAKE KUJITUNZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amewataka wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini kujitunza ili wacheze kwa muda mrefu na mafanikio.
  Waziri Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake kwenye Uwanja wa General Tyre jijini Arusha.
  Timu zilizokata utepe zilikuwa ni Alliance Queens ya Mwanza iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC ya Iringa.
  Katika uzinduzi huo Waziri Dk. Mwakyembe aliwataka wachezaji wa timu zote kujituma kwa juhudi zaidi kwa kuwa mpira wa miguu kwa sasa ni ajira kubwa sana kwa vijana.
  “Vijana wangu natambua mnapenda mpira wa miguu, naomba mzingatie vitu vitatu muhimu - nidhamu, juhudi na kujitunza,” amesema Waziri Dk. Mwakyembe akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred na viongozi wa FA Mkoa wa Arusha.
  Mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Waziri akiwa na viongozi hao leo ametembelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutazama maendeleo ya marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
  Mbali na uwanja  huo pia waziri alifanya ziara fupi kwenye viwanja wmbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanja cha FFU kwa Morombo, Arusha  ambapo aliwapongeza kwa ukarabati mzuri wa nyasi za kuchezea.
  Katika ziara nyingine Waziri pamoja na Viongozi wa TFF walitembelea shule ya Trust St. Patric Sports Academy ambacho ni kutuo cha kukuza michezo na timu zinazoshiriki ligi hiyo, zimeweka kambi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWAKYEMBE AWATAKA WACHEZAJI LIGI YA WANAWAKE KUJITUNZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top