• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 28, 2017

  SIMBA KUANZA NA URA, YANGA NA JKU UFUNGUZI ‘MAPINDUZI CUP’ 2018

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC itafungua dimba na URA ya Uganda katika michuano maarufu ya Kombe la Mapinduzi, Januari 2, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza Saa 2:15 usiku.
  Mahasimu wao, Yanga wataanza na JKU ya Zanzibar Januari 1, Uwanja wa Amaan pia, mchezo ambao nao utaanza Saa 2:15 usiku.
  Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan pia Januari 2, lakini kuanzia Saa 10:15 jioni. 
  Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku.        
  Simba imepangwa Kundi A pamoja na Azam FC, Jamhuri, Taifa ya Jang’ombe na URA ya Uganda, wakati Yanga imetupwa Kundi B pamoja na JKU, Mlandege, Zimamoto na Shaba.
  Simba itamenyana na Azam FC Januari 6, ikitoka kukipiga na Taifa ya Jang’ombe Januari 4, kabla ya kumalizia mechi zake za Kundi A Januari 8 na Jamhuri.
  Azam FC itacheza na Taifa ya Jang’ombe Januari 4 kuanzia Saa 10:15, kabla ya kumenyana na Simba na itahitimisha mechi zake za Kundi A kwa kuumana na URA Januari 8 Saa 10;15 pia jioni Uwanja wa Amaan.
  Baada ya mechi na JKU, Yanga watarudi tena uwanjani Januari 3 kwa mchezo na Shaba, Januari 5 na Zimamoto kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Mlandege Janauri 7 Uwanja wa Amaan.
  Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 10 na Fainali itakuwa Januari 13, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan kuanzia Saa 2:15 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA KUANZA NA URA, YANGA NA JKU UFUNGUZI ‘MAPINDUZI CUP’ 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top