• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 27, 2017

  MAREFA 18 WA TANZANIA WAPEWA BEJI ZA FIFA 2017-2018

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 katika msimu wa mshindano mwaka 2018.
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni Mfaume Ali, Heri Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina Zablon.
  Waamuzi Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli, Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na kwa wanawake Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace Wamala.
  Heri Sasii ni miongoni mwa marefa 18 waliotunukiwa beji za FIFA kwa msimu wa 2017-2018

  Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni  Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA 18 WA TANZANIA WAPEWA BEJI ZA FIFA 2017-2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top