• HABARI MPYA

    Wednesday, November 29, 2017

    KOCHA MPYA EVERTON, ALLARDYCE ASEMA WACHEZAJI HAWAJIAMINI TENA

    Sam Allardyce ni kocha mpya wa Everton kwa mswhahara wa Pauni Milioni 6 kwa mwaka PICHA ZAIDI GONGA HAPA


    RATIBA YA MECHI ZA EVERTON  

    Ligi Kuu ya England
    Jumatano West Ham (nyumbani)
    Jumamosi Huddersfield Town (nyumbani)
    Makundi Europa League 
    Desemba 7 Apollon Limassol (ugenini)
    Ligi Kuu ya England
    Desemba 10 Liverpool (ugenini)
    Desemba 13 Newcastle United (ugenini)
    Desemba 18 Swansea City (nyumbani) 
    KOCHA mpya wa Everton, Sam Allardyce amesema kwamba wachezaji wamepoteza hali ya kujiamini na ameiagiza klabu kusajili mbadala wa Romelu Lukaku. 
    Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 leo amethibitishwa kuwa kocha mpya wa Everton na mwanahisa mkuu wa klabu, Farhad Moshiri amemtaja kama kiongozi wa nguvu' na amemtabiria ataifikisha timu panapohitajika.'
    Lakini kuelekea utambulisho rasmi, Allardyce ameandika kwenye safu ya Paddy Power kutoa maoni yake juu ya kufanya vibaya kwa timu hiyo msimu huu.
    The Toffees wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England pointi mbili tu kutoka nafasi za kuteremka daraja, licha ya kutumia Pauni Milioni 140 kufanya usajili mzuri kwa lengo la kumaliza ndani ya sita bora. 
    Allardyce amekiri klabu ipo katika nafasi mbaya kwa sasa na amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kurejesha hali yab kujiamini. 
    Allardyce mwenye umri wa miaka 63, amerejea kutoka mapumzikoni leo na kukutana na Moshiri kusaini mkataba wa kufundisha Everton.
    Atakuwa anapokea mshahara Pauni Milioni 6 kwa mwaka katika miezi 18 ya mkataba wake na ataanza rasmi kazi jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Huddersfield Town Uwanja wa Goodison Park.
    Lakini leo atakwenda kushuhudia mchezo dhidi ya West Ham. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MPYA EVERTON, ALLARDYCE ASEMA WACHEZAJI HAWAJIAMINI TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top