• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 24, 2017

  ROBINHO AHUKUMIWA MIAKA TISA JELA KWA UNYANYASI WA KIJINSIA

  MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Robinho ameripotiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatua ya unyanyasi wa kijinsia.
  Taarifa nchini Italia zimesema kwamba nyota huyo wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, kwa pamoja na jamaa wengine watano, walidaiwa kumshambulia binti wa Kialbania katika klabu ya usiku mjini Milan Januari mwaka 2013. 
  Tukio hilo lilitokea wakati mchezaji mwenye umri wa miaka 33 sasa akiwa anachezea AC Milan baada ya kuondoka Etihad mwaka 2010.

  Robinho ameripotiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatua ya unyanyasi wa kijinsia 

  Marisa Alija Ramos, wakala na mwanasheria wa Robinho amesema tukio hilo lilitokea miaka mingi iliyopita na tayari mteja wake amekwishajitetea kwamba hakuwemo kweye sakata hilo.
  "Hatua zote za kisheria tayari zimechukuliwa kujibu maamuzi haya."amesema Robinho, ambaye kwa sasa anacheza Brazil ambaye hakuwpo mahakamani nchini Italia wakati wa hukumu hiyo.
  Ana haki ya kukata rufaa mara mbili na Italia inaweza kuchukua hatua juu ya hukumu hiyo baada ya taratibu hizo kufanyika.
  Mahakama ya Milan imeagiza muathirika alipwe Pauni 53,000 ambazo ni gharama za maumivu yake.
  Robinho alicheza kwa miaka minne klabu hiyo ya Serie A akicheza zaidi ya mechi 100 kabla ya kuhamia Ligi Kuu ya China mwaka 2015. 
  Kwa sasa anamalizia soka yake katika klabu yake Atletico Mineiro ya kwao, Brazil.
  Mchezaji huyo aliushitua ulimwengu baada ya kukamilisha usajili wake wa kwenda Man City siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha akisainiwa kwa Pauni Milioni 32.5 September 2008.
  Alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mmiliki mpya, Sheikh Mansour, lakini akaishia kucheza 53 appearances katika miezi yake 18 ya kuwa England.
  Robinho aliibukia Real Madrid akiwa kijana mdogo kabla ya kuhamia Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ROBINHO AHUKUMIWA MIAKA TISA JELA KWA UNYANYASI WA KIJINSIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top