• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 25, 2017

  OKWI AFURAHIA KUPATA MTOTO WA KIKE

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi amefurahia kupata mtoto wa kike baada ya mkewe, Florah Woods kujifungua jana.
  Binti huyo waliyempa jina Ella, anakuwa mtoto wa pili kwa Okwi na mkewe baada ya wa kiume, Aaron Elton ‘Okwi Jr’.
  Okwi ameposti picha ya mama na mtoto katika ukurasa wake wa Instagram sambamba na maelezo; “Habari fulani nzuri kushirikiana nanyi marafiki. Jana tumemkaribisha malkia mzuro katika ulimwengu huu. Wote, mama na mtoto wanaendelea vizuri,”.
  Okwi aliye katika msimu wake wa kwanza tangu ajiunge tena na Simba kwa mara ya tatu Julai mwaka huu kutoka SC Villa ya kwao, Uganda pia amempongeza mkewe, Florah kwa kujifungua salama na kumshukuru Mungu kwa zawadi hyo.
  Emmanuel Okwi akiwa na mkewe Florah Woods, ambaye amejifungua mtoto wa kike jana 
  Okwi ameposti picha hii kufurahia ujio wa malkia, Ella 
  Tayari Okwi na mtoto wa kiume, Aaron Elton ‘Okwi Jr’

  Okwi anatarajiwa kukosekana kwa mara ya pili kesho Simba ikiwakaribisha Lipuli ya Iringa katika mfululizo wa Ligi Ku ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Okwi aliumia mazoezini katika timu yake ya taifa, Uganda na hakuwpo Uwanja wa Umoja mjini Brazzaville wakati  The Cranes inalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Novemba 12, mwaka huu.
  Akakosekana pia Novemba 18 wakati klabu yake, Simba SC inawachapa 1-0 wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bata Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Baada ya mechi 10 za awali, Simba SC wapo kileleni kwa pointi zao 22, sawa na Azam FC wanaokaa nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 20 ni wa tatu na wamecheza mechi moja zaidi.
  Lakini Okwi anaongoza kwa ufungaji wa mabao, akiwa ametikisa nyavu mara nane na mara mbili zaidi ya Mzambia Obrey Chirwa wa Yanga na Mohammed Rashid wa Prisons, wakati Ibrahim Ajib wa Yanga, Eliud Ambokile wa Mbeya City na Habib Kiyombo wa Mbao FC wana mabao matano kila mmoja. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OKWI AFURAHIA KUPATA MTOTO WA KIKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top