• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 24, 2017

  WACHEZAJI WOTE REAL MADRID WAPEWA AUDI MPYA, KALI!

  WACHEZAJI wa Real Madrid wameendelea kufurahia udhamini wa kampuni ya Audi kwa kupewa gari mpya kila mwaka
  Na baada ya ushindi wa 6-0 Jumanne dhidi ya APOEL mjini Nicosia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa, Cristiano Ronaldo akivunja rekodi yake mwenyewe ya mabao kwenye michuano hiyo wachezaji wote wamepata gari mpya za kisasa.
  Lakini ni Ronaldo ndiye aliyepewa gari nzuri zaidi ya Audi kuliko wachezaji wenzake.
  Cristiano Ronaldo akiwa mbele ya Audi yake RS7, yenye thamani ya Pauni 150,000

  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alichagua Audi RS7 yenye thamani ya Pauni 150,000.
  Kocha Zinedine Zidane amepata Audi RS6, Sergio Ramos amechukua Audi R8 Spyder ambayo ni ya gharama zaidi, inayouzwa Pauni 200,000. 
  Nyota wengine wawili, Gareth Bale na Isco wamechukua Audi Q7 Sport, wakati Dani Ceballos na Mateo Kovacic wamechukua Q7 Sport.
  Baada ya hapo, wakashiriki mbio maalum za magari ya Audi, Formula E na beki wa kulia Dani Carvajal akaibuka mshindi akifuatiwa na Ramos na Marco Asensio katika nafasi ya pili na ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI WOTE REAL MADRID WAPEWA AUDI MPYA, KALI! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top